Usaidizi kabla ya kurudi

Ili kukusaidia wakati wa kurudi kwenye nchi yako, washauri wa kurudi nchini Austria watashughulikia mambo yafuatayo:

  • Ushauri kuhusu mitazamo katika nchi yako
  • Kutoa taarifakuhusu usaidizi unaowezekana
  • Mpangilio wa nyaraka za kusafiri
  • Ushughulikiaji wa gharama za kurudi
  • Mpangilio wa kurudi (ikiwa ni pamoja na tikiti za ndege)
  • Ikiwezekana, usaidizi kwenye uwanja wa ndege wa Vienna Schwechat wakati wa kuondoka na mpangilio wa usaidizi wa usafiri
  • Usaidizi wa kupokea msaada wa fedha
  • Ikihitajika, ubainishaji wa usaidizi wa matibabu kabla, wakati wa na baada ya safari

Huduma baada ya kurudi kwako

Mpango wa kujiunga ten awa „EU Reintegration Programme“ (EURP) unakupa msaada kwa ushirikiano na shirika la ndani wakati wa kujiunga tena baada ya kurudi katika nchi yako.

Usaidizi wa haraka
Kifurushi cha baada ya kuwasili cha thamani ya €615 kinatumika kwa msaada wa haraka baada ya kuwasili katika nchi yako na ni pamoja na huduma za haraka zifuatazo:

  • Kukaribishwa na mshirika wa kujiunga tena moja kwa moja kwenye uwanja wa ndege na kukabidhiwa kifurushi cha baada ya kuwasili: kadi ya SIM ya malipo ya mapema, bidhaa za usafi binafsi (mswaki, dawa ya meno, sabuni, shampuu, n.k.), chupa 1 ya maji, chakula 1 kilichopashwa moto (pia inapatikana kama vocha), mdoli kwa umri unaofaa kwa watoto
  • kuchukuliwa kwenye uwanja wa ndege
  • msaada wa kusonga mbele (kujipanga na kushughuliki gharama)
  • makao ya muda mfupi kwa hadi siku 3 baada ya kuwasili
  • usaidizi wa matibabu wa moja wa moja

Ikiwa huhitaji yoyote au unahitaji tu huduma Fulani za haraka, utapokea kiasi cha uwiano €615 pesa taslimu kutoka kwa mshirika wa ndani.

Msaada wa muda mrefu wa kujiunga tena
Zaidi ya hayo, utapokea kifurushi cha baada ya kurudi cha kiasi cha €2,000. Utapokea €200 ya kiasi hiki pesa taslimu na €1,800 kwa njia za manufaa kwa huduma kulingana na mpango wa kuungana tena tena utakaoundwa kwa usaidizi wa shirika la mshirika wa ndani wakati wa miezi 6 ya kwanza baada ya kurudi kwako.

Manufaa ya huduma yanayotolewa ya kifurushi cha baada ya kurudi ni pamoja na, miongoni mwa mambo mengine:

  • msaada wa kuanzisha biashara ndogo (kampuni)
  • shughuli za elimu na mafunzo
  • msaada wa kuingia katika soko la ajira
  • msaada wa usajili wa kuandamana na watoto shuleni
  • huduma za ushauri wa kisheria na utawala
  • kuungana tena na familia
  • usaidizi wa matibabu
  • msaada wa saikolojia na jamiii
  • msaada unaohusiana na nyumba na familia (kuweka samani)

Kwa maelezo zaidi na utumaji ombi, tafadhali wasiliana na ofisi ya karibu ya moja ya ofisi za ushauri wa kurudi ya Federal Agency for Reception and Support Services (BBU GmbH)


EU Reintegration Programme

Together with local partners, EURP supports returnees in their reintegration process in their countries of origin. For more information please visit the Frontex brochure, website, or contact a return counsellor.

Frontex Logo

We would like to inform you, that after activating, data will be transferred to the provider. Further information you will find in our data protection policy.

Taarifa za Jumla kuhusu Usaidizi wa Kujotolea wa Kurudi

We would like to inform you, that after activating, data will be transferred to the provider. Further information you will find in our data protection policy.

Msaada wa Kujiunga Tena kwa Wanaorejea kutoka Austria (BMI)


Get Return Assistance

Contact us, we help!